Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro Mrakibu wa Zimamoto (SF) Shabani Marugujo tarehe 25 Januari 2024 aliongoza Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo Kufanya maokozi ya watu baada ya kuzingirwa na Maji katika maeneo ya Mazimbu Road, Lukobe Tushikamane, Kihonda Mkundi, Kihonda Jakalanda, Azimio na Kihonda kwa Chambo

Maokozi hayo yamefanyika Kutokana mji wa Morogoro kukumbwa na Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
Mvua hizi zimesababisha Madhara kwa Wananchi wa mkoa huo ikiwemo vifo vya Watu watano (05), kubomoka kwa nyumba, uharibifu wa samani pamoja na miundombinu kwa ujumla
Katika maokozi hayo Jeshi limefanikiwa kuokoa kaya 157 zenye jumla ya zaidi ya watu 246 na kuzipeleka Maeneo salama

About The Author
Last modified: January 27, 2024