Visit Sponsor

Written by 4:58 pm BURUDANI Views: 4

WAZIRI SLAA: KWA AMANI TULIYOKUWA NAYO WATANZANIA NI TUNU

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

Waziri wa Mawasiliano na teknolojia,Jerry Slaa amesema kuwa amani tuliyonayo watanzania ni tunu kubwa ambayo inatakiwa kutunzwa.

Waziri Slaa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika tamasha la Mtoko wa Pasaka ambalo linafanyika katika ukumbi wa The super Dome jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa tamasha hilo ambalo lina kauli mbiu ‘Kwa maombi utashinda’ni kielelezo cha jitihada za kuendelea kuitunza amani tuliyonayo.

“Ukiangalia hata huko mitandaoni utaona adha ambayo wanaipata wananchi ambao nchi zao zina machafuko na hakika utaona kuwa amani tuliyonayo si ya kuichezea” amesema Slaa.

Tamasha la Mtoko wa Pasaka linafanyika usiku huu katika ukumbi wa The super Dome jijini Dar es salaam ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa injili akiwemo Rose Muhando,Christina Shusho,Solomon Mukubwa, na wengine wanatarajiwa kuhudumu katika tamasha hilo ambalo pia linaenda sambamba na maombi ya kuliombea Taifa.

About The Author

(Visited 4 times, 1 visits today)

Last modified: April 20, 2025

Close