
Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF),Deodatus Balile amewataka waandishi wa habari kuwa na vitambulisho vyao vya kazi hasa wanapotekeleza majukumu ya kuripoti KESI ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tundu Lissu
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 2,2025 katika ofisi za Makao Makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam amesema waandishi wanapaswa kuwa na alama kama kuvaa jaketi pamoja na kitambulisho cha kazi.
Balile amesema kwamba ni haki ya kila mwandishi wa habari kufanya kazi yake,mwandishi wa habari hapaswi kuzuiwa kufanya kazi yake ya kukisanya,kuchakata na kuhabarisha umma.
Aidha,amesema waandishi wanapaswa kufika mapema mahakamani ili wasikose nafasi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa. Habari Dar es Salaam,Bakari Kimwanga amesema ni jukumu la mwandishi wa habari kuwa salama wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwani usalama wa mwandishi ni jukumu lake.
About The Author
Last modified: May 3, 2025