Visit Sponsor

Written by 5:23 am KITAIFA Views: 21

TAMA YATANGAZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI KUFANYIKA TAREHE 5 SHINYANGA

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI

Kila Mwaka chama Cha wakunga Tanzania (TAMA) Kinaadhimisha siku ya kimataifa ya wakunga,chama hicho kinalenga fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wakunga Katika huduma za Afya ya uzazi,hasa Katika wakati wa majanga,migogoro,na changamoto zinazohusiana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Ameyasema hayo Leo 02 Mei 2025 Rais wa chama Cha wakunga Tanzania (TAMA) Beatrice Mwilike Amesema kuwa kila mwaka siku ya 5 mwezi wa 5 tunaadhimisha siku ya wakunga duniani na Tanzania mwaka huu kitaifa tutafanya maadhimisho hayo Katika mkoa wa shinyanga

“mkoa wa shinyanga tutaanza siku ya Tarehe 4 ambapo tutakuwa na Mafunzo mbalimbali ya kuwawezesha wakunga kwenye maeneo mbalimbali ya kuweza kutoa huduma mfano kupunguza utokaji damu Kwa wingi Kwa mama kujifungua maana imekuwa tatizo linaloongoza vifo vinavyotokana na uzazi”Amesema Mwilike

Ameongeza kuwa wameandaa warsha ya wakunga kuweza kupata ujuzi Zaidi na kupata maboresho ambayo yapo Katika utoaji wa huduma na kuweza kupata maboresho ambayo yapo Katika utoaji wa huduma Kwa mama ambae ameshajifungua ili kuzuia asitoke na damu nyingi na mwisho kuishia kupoteza maisha

Pia tutafanya warsha ya kuwafundisha wakunga namna ya kumuhudumia mtoto mchanga ambae amezaliwa vitu Gani vya kufanya na maswala ya unyonyeshaji Ili kuweza kuwapa uwezo wa kuwahudumia watoto wachanga na kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na vifo vya watoto wachanga vinavyotokea umri mdogo

“Siku ya Tarehe 5 tutakuwa na maadhimisho rasmi ya siku ya wakunga duniani Ambapo tutakuwa na maandamano ya wakunga”Ameongeza Mwilike

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Afya na uzazi mama na mtoto kutoka wizara ya afya Dkt  Mohammed Makuadi Amesema kuwa nipo hapa Kwa kuangalia namna ipi tunaweza kuboresha huduma za ukunga lakini hasa ukizingatia Katika nyakati zile ngumu za matatizo mfano mama mjamzito anapopata ugonjwa ambao usioweza kutibika wa kuambukiza

“Tunaangalia namna Gani tunamuezesha huyu mkunga akawa na mazingira Bora tukiangalia hapa nyumbani kidogo tumejitahidi sana Katika kuboresha mazingira nadhani mumeona mukienda pembezoni kunavituo vinavyotoa huduma za Afya hata hospital zilizojengwa zinapendeza sana ukienda hata kwenye wodi zetu zimebadilika”Amesema Makuadi

Hata Hivyo soti Abdallah ambae anaefanya kazi na shirika la msalaba mwekundu Tanzania association Katika kambi ya wakimbizi yarugusu Amesema Kwa mazingira ambayo tunayofanya kazi tunatoa huduma ya afya Kwa wanajamii tunao wakunga mbalimbali tukielekea kuazimisha siku ya wakunga duniani ya mwaka 2025

Amesema kipindi Cha nyuma wakunga walikuwa hawapewi thamani,heshima lakini ukiangalia Kwa Sasa wakunga wanaheshimika sana na wanafanya kazi za muhimu sana “ukiangalia huduma ambazo tunazozitoa kule kambini kalibia vizazi 620 Kwa mwezi wanatoa huduma Kwa ufasihi kabisa Kwa msingi Kwa Sasa hivi wakunga wanathaminika sana Katika jamii tunayoiidumia”Amesema Abdallah

About The Author

(Visited 21 times, 21 visits today)

Last modified: May 3, 2025

Close