Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
_Litachukua Wanafunzi 80 na kuwahudumia pamoja bure badala ya kwenda na kurudi ambako ni hatari kwa watoto wenye mahitaji maalum._
Watoto Walemavu na Wenye mahitaji maalum wanahitaji uangalizi maalumu na wa karibu. Tarafa ya Katerero kwenye kata za Nyakibimbili, Ibwera, Kaibanja n.k zina watoto wengi Walemavu na Wenye mahitaji Maalum lakini kutokuwepo kwa bweni la kuwakusanya wote pamoja na kuwahudumia kwa uangalizi kulifanya watoto wengi Walemavu wakose haki yao ya kupata elimu na wengine kuacha shule kwasababu ya umbali.
Kwa kuliona hilo, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ikatoa milioni 128 kujenga bweni la Kisasa Shule ya Msingi Lyamahoro A iliyopo kata ya Nyakibimbili ili kuwalea watoto hawa huku wakipata haki yao ya elimu badala ya kwenda na kurudi ambako kwa watoto walemavu ni changamoto kubwa.
Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero mkoani Kagera, Bwanku M Bwanku Jana Jumatano akiwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Edmund Mushema, Mtendaji wa Kijiji cha Nyakibimbili, John Chonya, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata Bi Mgala Masatu na Mwl anayehudumia watoto hao wamekagua ujenzi wa bweni hilo ambalo kwasasa limekamilika likihitaji vitanda tu na miundombinu ya maji na umeme ili wanafunzi waanze kulitumia ambapo Afisa Tarafa Bwanku ameahidi kusukuma kuhakikisha mambo yaliyobaki yanakamilishwa ili wanafunzi waanze kulitumia.
Serikali ya Rais Samia kupitia kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imejenga bweni hili ili kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalumu kupata haki yao ya kupata elimu kwa viwango vya kisasa bila changamoto yoyote.
“Zamani ilikua nadra sana kukuta mradi mkubwa kama huu kijijini ndanindani huku, mara nyingi miradi hii ungeikuta zaidi mijini lakini sasa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan miradi hii imejaa kote mijini na vijijini.” Alisema Afisa Tarafa Bwanku
About The Author
Last modified: May 3, 2025