Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau wa Elimu ya Ualimu nchini Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mradi wa kuimarisha mafunzo ya elimu kwenye Vyuo vya Ualimu 35 vinavyomilikiwa na Serikali nchini (TESP) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada kwa gharama ya bilioni 78, umenikiwa kukarabati vyuo nane na kujenga chuo kipya cha Kabanga mkoani Kigoma ambacho kilifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kimekuwa ni mfano wa taasisi za Tanzania ambazo zinaweza zikajinfunza namna ya kujenga kwa kuzingatia mazingira.

Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo wakati akifungua Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kupitia mradi huu ambao pia umesaidia kuangalia masuala ya usawa wa kijinsia, Vyuo hivyo vya Ualimu sasa vina vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwani wamesaidia kununua vitabu, laptop, printers na kuwafanya wakufunzi waweze kufundisha kwa njia ya TEHAMA. Pia vyuo 15 vya Ualimu vimeshaunganishwa na Mkonga wa Taifa na sasa wanapata mtandao kirahisi unaowawezesha pia kupata hata mada za kufundisha na wanafunzi wanaweza kupata taarifa mbalimbali kupitia mkonga huo na vifaa vya TEHAMA vilivyopo vyuoni.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula, akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha wadau wa Elimu ya Ualimu Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam Oktoba 30, 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo alipokuwa akifungua kikao cha siku mbili kwa wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu nchini ambapo alisema Rais Samia ameifanya elimu kuwa kipaumbele kwa kufanya uwekezaji mkubwa ikijumuisha utolewaji bure kuanzia elimu ya awali hadi sekondari ambayo inahakikisha upatikanaji elimu ya msingi kwa wasichana na wavulana wote wa Kitanzania, huku kauli mbiu yake ikiwa “Hatumuachi mtu yeyote nyuma”.

Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo wakati akifungua Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
“Ninatoa pia shukrani za dhati kwa Serikali ya Canada kwa kuifanya Elimu ya Ualimu na elimu kwa ujumla kama kipaumbele katika kusaidia hapa nchini. Kwa upande wa TESP jumla ya dola milioni 53 za Canada zimetolewa kwa ajili ya mradi huu, kwa niaba ya Serikali nirudie tena, nina wahakikishia ushirikiano wa kimataifa wa kiwango cha juu ili kuweza kuimarisha mahusiano yetu, lakini pia kuhakikisha malengo ya mradi huu yanafikiwa,” alisema Prof. Carolyne.

Mwakilishi wa Serikali ya Canada Mhe.Helen Fytche akizungumza katika ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Aidha Nombo amesema kuwa malengo makuu ya mkutano huo wa wadau wa Elimu ya Ualimu kwanza ni kushirikishana uelewa wa nini yamekua ni mafanikio na changamoto ya mradi wa TESP na sekta nzima ya Elimu ya Ualimu kwa ujumla, pia kushirikishana juu ya uelewa kuhusu mabadiliko na matokeo ya sera mpya ya elimu na mafunzo na namna ambavyo mitaala ya Elimu ya Ualimu itaenda kutolewa kwa kuzingatia mabadiliko yaliyopo katika mitaala hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Elimu ya Ualimu wakati wa Ufunguzi wa kikao cha wadau hao Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
“Lengo lingine ni kuboresha utendaji uliyopo ili kuleta ujifunzaji endelevu miongoni mwa wadau, tunaamini katika mijadala yao wataleta ujifunzaji endelevu miongoni mwa wale ambao wanafundishwa na wale ambao wanatoa mafunzo na wale ambao wananufaika na mafunzo hayo kwa ujumla. Pia watajenga na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa Uyuo vya Ualimu na wadau ili kuboresha mipango na mikakati ya utoaji wa Elimu ya Ualimu kwa ujumla.
“Ni matarajio yangu kwamba, mkutano huu utawezesha kila mshiriki kuwa na nafasi ya kujadiliana juu ya matokeo ya TESP, changamoto ambazo zimejitokeza katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi na hata pia kutafuta suluhisho kwa changamoto mbalimbali, lakini muhimu zaidi kuona namna gani mafanikio hayo yanawezekana kuendelea kuwepo hata baada ya mradi.” alisema.
Prof. Carolyne alisema, lengo kuu la TESP ni kuboresha Elimu Msingi kwa wasichana na wavulana nchini kupitia kuimarisha uwezo wa rasilimali watu katika Vyuo vya Ualimu na shule, kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuwezesha upatikanaji wa rasilimali za kujifunza na kufundishia vyuoni, lakini pia kuboresha miuondombinu katika vyuo kupitia ujenzi na ukarabati wa majengo.
About The Author
Last modified: October 30, 2023