Visit Sponsor

Written by 5:15 pm KITAIFA โ€ข Views: 2

NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI KIPAUMBELE CHA SERIKALI – MHANDISI MRAMBA



๐Ÿ“Œ *Ashiriki Marathon ya Kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia*

๐Ÿ“Œ *Asema Nishati Safi ya Kupikia itapunguza uharibifu wa mazingira na kulinda afya*

Katibu Mkuu wa Wizara Ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba amesema kuwa, suala la upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ni moja ya vipaumbele vya nchi na kwamba Serikali inahakikisha kuwa Mpango Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia unatekelezwa kwa kasi na kwa umakini ili kutimiza azma ya nchi kuhama kutoka matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia kwenda kwenye nishati safi.

Amesema hayo tarehe 17 Mei, 2025 jijini Dar es Salam wakati akishiriki Marathon ya Nishati Safi ya Kupikia oiyofanyika katika viwanja wa Oysterbay..

โ€œSerikali imeamua kwenda nalo kasi suala hili la nishati safi ya kupikia ili kuepusha uharibifu wa mazingira kwani nishati ambayo si salama kama kuni na mkaa inatumika kwa kiasi kikubwa kwa kupikia hivyo tukitekeleza Dira hii, kwa kiasi kikubwa tutapunguza uharibifu wa mazingira pamoja na kulinda afya za wananchi.โ€ Amesema Mramba

Mha. Mramba, amewapongeza waandaaji wa Marathon hiyo Shirika la Wafanyabishara Wanawake (TABWA) ambayo imelenga kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia  kwa Wananchi.

Aidha, amewaasa  Wadau mbalimbali kuzidi kujitokeza ila kuzidi kuendeleza mikakati ya kusambaza elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Watanzania wengi zaidi.

About The Author

(Visited 2 times, 2 visits today)

Last modified: May 17, 2025

Close