Visit Sponsor

Written by 6:34 am KITAIFA Views: 5

NIDA WAFANYAMSAKO WA KUWAKAMATA WALE WOTE WANAOTENGENEZA VITAMBULISHO BANDIA

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  katika kutekeleza  operesheni imefanikiwa kumkamata Danford Mathias Mkazi wa Chalinze mkoani Pwani aliyekuwa akijihusisha na utengenezaji na uchapishaji wa vitambulisho vya Taifa ambavyo ni bandia.

‎Hayo yamebainishwa na  Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano NIDA Jofrey Tengeneza wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 02, 2025 Jijini Dar es Saalam,ambapo  amesema kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na wimbi kubwa la watu walioibuka na kuwatapeli wananchi kwa kujinadi kuwa wanaweza kuwapatia huduma zitolewazo na NIDA.

‎”Kutokana na  kukithiri kwa vitendo hivyo, walianzisha operesheni maalum  ya kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria  wale wote wanaojihusisha na utapeli na Aprili 23 2025, majira ya saa 9:00 Alasiri kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walifanikiwa kumkamata mtu huyo”,alisema Tengeneza

‎Aidha amesema NIDA  kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tulimuwekea mtego na kufanikiwa kumkamata pamoja na vifaa vyake baada ya kutengeneza kitambulisho kwa malipo ya shilingi 10,000.

‎”Mtuhumiwa huyu alikuwa akitengenezea wateja vitambulisho feki katika steshenari yake iitwayo Bwanga studio iliyopo Msata Chalinze kwa malipo ya kati ya Sh. 6,000 na 10,000.Katika kutengeneza vitambulisho hivyo feki, Danford Mathias hutumia kitambulisho chake halali cha NIDA na kukiscan na kisha kukiingiza kwenye mfumo wa Adobe na kufuta taarifa zake, na kubandika taarifa za mteja ikiwemo Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN), picha, majina, Saini na kuwawekea tarehe zinazoonyesha ukomo wa matumizi ya kitambulisho hicho yaani expiry date,” amesema.

‎Tengeneza amewakumbusha  wamiliki wote wa maduka ya steshenari kutokujihisisha kwa namna yeyote ile na utengenezaji au uchapishaji wa vitambulisho feki vya Taifa kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na ni kinyume cha Sheria ya Usajili na Utambuzi Sura ya 36 ya mwaka 2012, Kanuni ya Usajili na Utambuzi wa Watu ya Mwaka 2014 na Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura Na. 16 mwaka 2022.

‎”Niwakumbushe wananchi wanaoamua kwenda katika maduka ya steshenari kwa lengo la kutengenezewa vitambulisho vya Taifa kwanza, wafahamu kuwa vitambulisho hivyo ni feki,hivyo kumiliki kitambulisho cha namna hiyo ni kosa na utakapokamatwa nacho utafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

‎”Pili ni kosa kwa mtu kutoa pesa ili kutengenezewa kitambulisho hicho kwani kitambulisho halisi ni kile kinachotengenezwa na kuchapisha na NIDA, na mara ya kwanza hutolewa bure bila malipo yoyote,” amesema

‎Hata hivyo ,ameongeza kuwa operesheni hiyo ni endelevu na inafanyika nchi mzima kwani utapeli wa aina hiyo unafanyika sehemu mbalimbali nchini.

‎Sambamba na hayo ,Tengeneza amesema kuwa kuanzia jana saa 6:00 usiku wameanza  kufungia Namba za Utambulisho (NIN) kwa wale ambao walitumiwa ujumbe mfupi wa simu za mkononi kuwataka wakachukue vitambulisho vyao lakini hawakujitokeza kuchukua.

‎Katika hatua nyingine kama tulvyokwisha. Kutangaza kuwa ifikapo Mei 01, 2025 tutafunga matumizi ya Namba za Utambulisho wa Taifa  NIN na kuanzia jana tumeanza kuzifungia, hata hivyo tumepokea simu nyingi watu wakiuliza itakuaje baada ya kufungiwa. Sasa nitumie fursa hii kwa mara nyingine tena kuwafahamisha wananchi kuwa namba inapofungwa haina maana ndiyo basi Utambulisho umefutwa, utakapokuja kuchukua kitambulisho chako namba yako inahuishwa na kuanza kutumika tena.

‎Amemalizia kwa kuwataka wananchi waendelee kujitokeza kwenda kuchukua vitambulisho vyao hata kwa wale ambao hawajapata ujumbe mfupi wa simu (sms) waende pia

About The Author

(Visited 5 times, 5 visits today)

Last modified: May 3, 2025

Close