
Na Yohani Gwangway
Mtaalamu wa masuala ya Uchumi na mchambuzi Dr. Bravious Kahyoza amesema kuwa kumeongezeka ushirikishwaji wa wananchi katika masuala yanahusu hatma ya nchi yao ikilinganishwa na miaka 25 iliyopita katika mahoajiano yake aliyofanya na kituo cha habari cha Star TV.
Dr. Kahyoza alikuwa akizungumzia ushirikishwaji wa wanchi katika masuala ya kitaifa kama utengenezaji wa bajeti, utengenezaji katika dira ya maendeleo ya taifa na masuala mengine yanayogusina na maendeleo hapa nchini.
“Kuna mabadiliko makubwa, kuna uhusishwaji mkubwa hivi sasa tofauti na tulivyofanya miaka 25 iliyopita. Ni kuendelea kushirikisha watu katika kila hatua, hasa kwenye mchakato wa Bajeti. Sasa hivi mtandao wa ‘International Budget Partnership’ unaonesha kwamba wananchi wa Tanzania wanaushiriki mdogo katika utengenezaji wao wa Bajeti ukilinganisha na nchi zinazotuzunguka.” Alisema Dr. Kahyoza.
Ikiwa hivi karibuni Tanzania iliandaa Dira ya amendeleo ya Taifa katika mjadala uliohusisha makundi mabalimbali, mtaalamu huyu anaona kuwa kama taifa ilikuwa muhimu kuwa na Dira hiyo ili kujua ni wapi tunataka kufika.
“Dira inakuonesha ni wapi unataka kuelekea, inakuonesha wapi ulikotoka na ufanye nini ili uweze kuendelea. Kwa hiyo ni jambo muhimu sana. Utaona Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 imetusaidia katika maeneo fulani, na tunapotengeneza ya 2050 tutakuwa tumejifunza. Dira ni muhimu.”

Katika hatua nyingine Mtaalamu huyo wa Uchumi ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa miongoni mwa wakufunzi wa mafunzo ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) yanayoratibiwa na kituo cha Ubia kati ya sekta ya Umma na binafsi PPPC amesema kuwa anaona kuna faida kubwa ya uchumi unaotekelezwa kwa mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuvutia mitaji na kuongeza ufanisi kwenye uchumi wa taifa
“Faida za Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ni Kuvutia mitaji ili kuwekeza kwenye maeneo ambayo serikali ingekuwa na ufinyu wa fedha kupata mitaji hiyo, Kuongeza ufanisi kwenye uchumi wetu, Inawezesha kugatua mitaji kuwafikia watu wa chini na kusadia kupunguza deni la nchi.”
Dr. Kahyoza ameeleza zaidi kuwa ilikuwa na hatua nzuri kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuanzisha Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPPC ambacho kiko chini ya Mkurugenzi wake Mhe. David Kafulila
“Umuhimu ni mkubwa sana. Serikali inaweza kushirikiana na wadau wengine ili kuweza kufanya shughuli hizo za kiuchumi. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alichukua hatua madhuhuti za kutengeneza Kituo cha Ubia kati Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC) chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Mhe. David Kafulila”
Hivi karibuni Kituo hicho kilihitimisha zoezi lake la kutoa mafunzo katika mikoa yote nchini Tanzania mafunzo yaliyolenga kuibua miradi ya Ubia kati ya sekta ya Umma na binafsi katika mikoa husika.
Maoni ya Dr. Kahyoza kuhusu masuala ya uchumi
Katika mahojiano hayo Dr. Kahyoza alipoulizwa kuhusiana na swala la ugumu wa maisha mbao wengi wamekuwa wakiulalamikia alisema kuwa katika kundoa umaskini wa watu dhana ambayo haiwezi kupuuzwa ni madhara ya muda mrefu ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei na ghara ya maisha kwa Ujumla. Licha ya hali ilivyo mtaalamu huyo wa uchumi anaona kuwa juhudi zilizopo zinaweza kusaidia kupunguza uamskini kwa watanzania akitolea hatua zilizopigwa kwenye sekta ya kilimo.
“Serikali imechukua hatua za kutosha kuhakikisha gharama za maisha zinahimilika. Mwaka 2021 wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani, Bajeti ya Wizara ya Kilimo ilikuwa chini ya Tsh. Bilioni 300, ndani ya miaka minne imevuka Tsh. Trilioni 1. “
Kuhusiana na suala la wageni kuchukua sekta muhimu hasa katika masuala mabyo yangeweza kufanywa na watanzania Dr. Kahyoza ameonesha wasiwasi wake akisema kuwa taifa linahitaji kulinda nafasi ya wananchi wa ndani
“Tatizo hilo limekuwepo. Kwenye kufungua uchumi ni lazima uangalie mantiki ya uchumi wa ndani, na kwa kweli nchi zote ambazo zimeweza kwenda vizuri na kuchukua hatua za kiuchumi na kuondoa umaskini wa watu zimekuwa zikilinda nafasi ya wananchi wa ndani ili kuwekeza kucheza kwenye soko.”
Maoni kuhusu safari za nje.
Alipoulizwa kuhusiana na masuala ya safari ya nje hasa kwa kufananisha maamuzi ya Rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli kuzuia safari za nje na maamuzi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kusema kuwa nchi inahitaji kufunguka, Dr. Kahyoza alikuwa na haya ya kusema
“Ni vigumu kusema ilikuwa ni hatua mbaya iliyopita, au hii ni hatua nzuri kuliko nyingine. Lakini nizungumze kwa sasa ni kwamba kumekuwepo na matokeo makubwa, kati ya mwaka 2021 mpaka sasa, biashara ya kimataifa yetu imekuwa na ongezeko la wastani wa USD Bilioni 8 kila mwaka. Hiki ni kiwango ambacho hakikuwahi kufikiwa katika hatua nyingine yoyote kwa mwaka mmoja. Utaona kuna matokeo kwa maana bidhaa zenu zinazozalishwa Tanzania zinaweza kwenda.”
Maoni kuhusu hali ya kisiasa.
Katika kuangazia hali ya kisiasa nchini Tanzania na ikiwa tayari taifa lina siasa safi, Dr. Kahyoza alisema kuwa kuna mazingira ya kisiasa yanahitaji kuboreshwa ili kufikia malengo ya kitaifa huku akionesha matumaini kwa hatua ya Rais Samia ya kusema kuwa kunahitaji “Reforms” katika siasa za nchi
“Ninachoweza kusema ni kwamba tunahitaji kuboresha mazingira yetu ya kisiasa, nadhani watu wengi wanakubaliana juu ya hilo, viongozi wa nchi wanakubaliana juu ya hilo. Ndiyo maana Rais aliyepo madarakani alipoingia alisema anataka kufanya mabadiliko na mageuzi yaani ‘Reforms’. Rais ashatuonesha njia.”
Joto la uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 likiwa limeshaanza katika baadhi ya vyama vya siasa hasa kwa wenye nia ya kugombea kuonesha matarajio yao ya kugombea, Dr. Kahyoza aliyoulizwa kama anataka kuingia rasmi kwenye siasa na kugombea ubunge mwaka huu alikuwa na haya
“Nafikiri kwa hali ilivyo hivi sasa ya nchi yetu, Rais anazungumza sana kuhusu kubadilisha uchumi wetu, kujenga nchi ambayo inakimbia kwa kasi, bila shaka watu wa aina yetu sisi wanauchumi ambao tunaweza kutafakari mambo haya vizuri na kuweza kumsaidia kusukuma nchi mbele, unaweza ukawa ni uamuzi wa msingi.”
About The Author
Last modified: May 20, 2025