Visit Sponsor

Written by 10:21 am KITAIFA Views: 115

DKT. BITEKO AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU PSSSF

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 3, 2023.

PSSSF, ni miongoni mwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

CPA. Kashimba alipata fursa ya kumpongeza Dkt. Biteko kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo Agosti 30, 2023 na kula kiapo Septemba 1, 2023.

Pia CPA. Kashimba alitumia fursa hiyo kujitambulisha ikiwa ni pamoja na kumueleza utekelzaji wa majukumu ya Mfuko kama yalivyoainishwa kwenye Sheria namba 2 ya mwaka 2018, iliyoanzisha PSSSF, ambayo ni pamoja na Kuandiskisha Wanachama, Kukusanya Michango, Kuwekeza na kulipa Mafao.

About The Author

(Visited 115 times, 1 visits today)

Last modified: November 4, 2023

Close