Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza rasmi kuwepo kwa mkutano mkuu maalumu wa CCM Taifa, utakaofanyika Mei 29 hadi 30,mwaka huu Jijini Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 17, 2025,nJijini Dar es salaam na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM) Taifa, CPA. Amos Makalla,wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakuzitaja ajenda tatu zitakazowasilishwa katika mkutano huo,huku ajenda kuu ikiwa ni kupokea na kuzindua rasmi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/2030,itakayotumika katika kuinadi CCM kwenye kipindi cha kampeni za chama.
CPA Makalla amesema ajenda nyingine ni kupokea Ilani ya CCM ya kipindi cha miaka mitano 2020/ 2025 Tanzania Bara na Zanzibar na huku ajenda nyingine ikiwa ni kufanyia marekebisho madogo ya katiba ya chama hicho.
Pia amesema kuwa, CCM inaamini katika kushinda kwenye uchaguzi mkuu kutokana na kuwa na Ilani inayokidhi mahitaji ya wananchi katika vipindi vyoto iliyoshika madaraka.
“Napenda kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo katika sekta ya afya, elimu,miundombinu ya barabara,maendeleo ya jamii na nyingine”amesema CPA Makalla.
About The Author
Last modified: May 17, 2025