Visit Sponsor

Written by 4:57 pm KITAIFA Views: 32

BASHUNGWA: SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA MASLAHI YA WALIMU

Karagwe – Kagera.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa(Mb) amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha maslahi ya Walimu nchini na imedhamilia kutatua na kumaliza malalamiko na kero za Walimu nchini ikiwa ni pamoja na madaraja na stahiki zao mbalimbali.

Amesema hayo tarehe 27 Oktoba 2023 wilayani Karagwe mkoani Kagera katika Sherehe ya kuadhimisha kilele cha siku ya Mwalimu Duniani na miaka 30 ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) yenye kauli mbiu “Walimu Tuwatakao, kwa Elimu Tuitakayo, Lazima Kutatua Uhaba wa Walimu”

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya mama yetu, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu imeendelea kulipa Madeni ya Watumishi ya Mishahara na yasiyo ya Mishahara kwa nyakati tofauti” amesema Bashungwa

Aidha, Bashungwa amesema tangu Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Serikali imeajiri jumla ya walimu 29,879 wa Shule za Msingi na Sekondari nchini ambapo takwimu zinathibishisha Rais wetu anavyothamini sana kada ya Walimu.

Bashungwa amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo tangu aingie halmashauri ya wilaya Karagwe imeshapokea Bilioni 3.113 kuboresha elimu ya msingi na Bilioni 5.514 kuboresha elimu ya Sekondari.

Kuhusu Kanuni ya Malipo ya Mkupuo na Malipo ya Pensheni kwa Wastaafu (Kikokotoo), amesema Serikali ya imeendelea kuwa sikivu na kuwathamini walimu wastaafu, na watumishi wote waliotumikiaa Taifa hili.

Kadhalika, Bashungwa amewapongeza Walimu wa kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na maarifa na amewasisitiza kuzingatia maadili ya kazi ya ualimu wakati wanapotekeleza majukumu yao

“Niwaahidi tutaendelea kushirikiana, Jambo lenu ni Jambo la Serikali pia ni jambo langu mimi kama Mbunge wa Jimbo la Karagwe, vile vile niwaahidi wakati mtakapojiandaa kufanya Bonanza lenu, nitaleta vifaa vya michezo katika tarafa zote” amesema Bashungwa

About The Author

(Visited 32 times, 1 visits today)

Last modified: October 27, 2023

Close