Visit Sponsor

Written by 3:06 pm KITAIFA Views: 151

TANZANIA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUU NCHI WANACHAMA KUTOKA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia)  akifafanua jambo  wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu maandalizi ya  Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma (kushoto) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Dkt. Jim  Yonazi.       

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika utakaofanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 23 hadi 27 mwaka 2023.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano huo kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu masuala muhimu yatakayojadiliwa.

Baadhi ya Makatibu Wakuu na Wawakilishi wakifuatilia kikao kuhusu maandalizi ya  Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi amesema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema Nchi  wanachama wa jukwaa hilo ni pamoja na  Kenya, Uganda, Namibia, Zimbabwe, Eswatini, Msumbiji, Seychelles, Botswana.

Nchi nyingine ni Angola, Zanzibar, Malawi, Lesotho, Mauritius, Zambia na Afrika ya Kusini ambapo mkutano huo utafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Jukumu la Mahakama za Nchi Wanachama katika Utatuzi wa Migogoro chini ya Utangamano wa eneo Huru la Biashara la Afrika: Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa kwa Ufanisi katika Utoaji Haki”

About The Author

(Visited 151 times, 1 visits today)

Last modified: September 5, 2023

Close