
Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Mtandao wa mawasiliano wa Airtel umefungua maduka manne mapya katika maeneo ya Sinza Vatican, Kawe, Mikocheni na Mwananyamara, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kusogeza huduma karibu zaidi na wateja wake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika katika duka la Sinza Vatican, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Bi. Adriana Lyamba alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa kampuni katika kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

“Hatutaishia hapa; tunaendelea kupanua huduma zetu hadi maeneo ambayo bado hayajafikiwa ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma kwa urahisi na ufanisi,” alisema Bi. Lyamba.
Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa Maduka ya Airtel Tanzania, Bw. Gasper Ngowi, alisema kuwa maduka hayo yatatoa huduma zote muhimu zinazopatikana katika makao makuu ya kampuni hiyo, ikiwa ni pamoja na usajili wa laini mpya, kurudisha laini iliyopotea, huduma za intaneti, na huduma nyinginezo za mawasiliano.

“Huduma katika maduka haya zitapatikana kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni, ili kutoa nafasi kwa wateja wengi zaidi kuhudumiwa kwa wakati unaowafaa,” aliongeza Bw. Ngowi.
About The Author
Last modified: May 15, 2025