Visit Sponsor

Written by 7:05 pm KITAIFA โ€ข Views: 8

GAVANA BWANKU ASHIRIKI MAHAFALI YA KIDATO CHA 6 LYAMAHORO, AELEZA WANANCHI KAZI KUBWA YA MAENDELEO ILIYOFANYWA NA SERIKALI ENEO LAO

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

_๐Ÿ“ŒAwaeleza wahitimu Serikali ilivyoongeza Bajeti ya Mikopo kutoka Bilioni 570-787 na Boom kutoka Tshs 8500 hadi 10,000 ili wasome bila shida._

Juzi Ijumaa Mei 16, 2025 Shule ya Sekondari Lyamahoro iliyopo Kata ya Kaibanja ndani ya Tarafa ya Katerero mkoani Kagera ilikua ikifanya mahafali yake ya kwanza ya kidato cha 6 toka Shule hiyo ipate kidato cha 5 na 6 mwaka 2023. Afisa Tarafa (Gavana) ya Katerero, Bwanku M Bwanku alishiriki mahafali hayo ambapo mgeni rasmi alikua Mfanyabiashara Assa Obeid.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Wilaya ya Bukoba Vijijini Bi. Joyce Justinian na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Jasson Lwankomezi walikuwepo pia.

Gavana Bwanku alitumia hadhara hiyo iliyokua na wazazi, wanafunzi na wananchi mbalimbali kuwaeleza kazi kubwa ya maendeleo iliyofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Kata ya Kaibanja ikiwemo kujenga zahanati mpya ya Kazinga, kupandikiza samaki milioni 1.5 kwenye Ziwa Ikimba linalonufaisha Kata hiyo ili wananchi wapate samaki wengi na wakubwa zaidi kuliko ilivyokua wanapata dagaa tu.

Pia, Gavana Bwanku aliwaeleza pia jinsi Serikali ya Rais Samia ilivyofanikisha maboresho makubwa ya Shule yao ya Lyamahoro ikiwemo kuipandisha hadhi na kuwa na kidato cha 5 na 6, ujenzi wa mabweni mawili, madarasa 6 kwa mpigo na bwalo kubwa vyote vikigharimu zaidi ya milioni 500. Hiyo ni pamoja na kuiweka kwenye mpango wa ujenzi wa lami barabara muhimu na kubwa ya Kyetema hadi Kyaka inayopita kwenye Kata hiyo ya Kaibanja.

“Nyinyi wenzetu wa Kidato cha 6 mnaohitimu ili mwende Vyuo Vikuu, Serikali ya Rais Samia imeongeza Bajeti ya Mikopo kwa ajili yenu Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu kutoka Bilioni 570 hadi sasa 787 na kuongeza pesa ya kujikimu (Boom) kutoka Tshs 85,000 hadi 10,000 ili mkifika Vyuo Vikuu mnakoenda mpate Mikopo ili msome vyema bila kuumiza wazazi mana Serikali ya Rais Samia imegharamia masomo yenu yote ya Vyuo Vikuu”. Gavana Bwanku aliwaeleza Wahitimu hao

“Kata ya Kaibanja na Taifa letu zima limepata maendeleo makubwa sana chini ya Rais Samia, mafanikio yote haya na mengine makubwa yanayokuja yanachochewa na uwepo wa amani kwenye Taifa letu, hivyo niwaombe wananchi wenzangu tuendelee kutunza amani yetu hasa mwaka huu wa Uchaguzi na tusitoe mwanya kwa wanasiasa ama watu wanaohubili chuki na vurugu ndani ya Taifa letu.” Alisisitiza Gavana Bwanku wakati akiongea kwenye mahafali hiyo

About The Author

(Visited 8 times, 1 visits today)

Last modified: May 19, 2025

Close