Visit Sponsor

Written by 8:01 am BURUDANI โ€ข Views: 40

STAR TIMES YATAMBULISHA GARI LA MSHINDI WA SHINDANO LA BINGWA

Na Beatrice Kaiza

IKIWA zimebaki siku kadhaa kuelekea Fainali ya Shindano la Bingwa Kampuni ya StarTimes imetambulisha zawadi ya gari aina ya Toyota crown yenye thamani ya Sh milioni 20 itakayotolewa kwa mshindi wa shindano la bingwa msimu wa pili katika fainali itakayofanyika wiki ijayo.

Shindano la bingwa msimu wa pili lilizinduliwa tangu Julai mwaka huu na kushirikisha washiriki 24 ambao ni maarufu mitandaoni waliokaa katika jumba moja maalum kuonesha uhalisia wa maisha yao na kuoneshwa kwenye televisheni ya TV3.

Akizungumza a waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko a Maudhui wa StarTimes, David Malisa amesema kuwa mshindi wa kwanza sio tu ataondoka na gari Bali kuna fedha taslimu ambazo itakuwa ni kama ‘surprise’ zitakazoenda kumsaidia kuendesha maisha
yake.

“Tunawashukuru Watanzania wanaoendelea kufuatilia vipindi vyetu, msimu huu wa sikukuu tunawaambia Lipa Tukubusti, lipia vifurushi tofauti upate nyongeza na kushuhudia fainali hi kuona bingwa ni nani msimu huu.

Pia, amesema shindano hilo limekuwa ni daraja la kufunguka kwa fursa nyingi kwani wapo watakaopata ubalozi wa bidhaa kutoka katika makampuni mbalimbali ya biashara.

Kwa upande wake, Meneja Mradi wa shindano hilo, Ombeni Phiri amesema washiriki wamebaki 12 walioingia fainali hivyo, wataendelea kuchuana hadi wiki ijayo.

โ€œMshindi mmoja ataondoka na gari Toyota Crown mpya, kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa pili na tatu,โ€ amesema Phiri.

Pia ameongeza kuwa washiriki hao wakiwa ndani ya jumba hilo walijifunza vitu vingi ikiwemo fursa za kutumia mitandao ya kijamii kujinua kiuchumi na kukuza majina yao.

About The Author

(Visited 40 times, 1 visits today)

Last modified: December 10, 2023

Close