Visit Sponsor

Written by 1:39 pm KITAIFA Views: 65

MAKONDA AMTEMBELEA MUFTI, AFANYIWA DUA MAALUM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda leo  Desemba 1, 2023 amemtembelea na kumshukuru Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakar Zuberi kwa kumuombea na kua nae katika nyakati zote alizopitia.

Makonda amefanya hivyo ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano na viongozi wa dini katika kufanya kazi kwani anatambua ndio sehemu kubwa inayochochea uwepo wa Amani katika Taifa kutokana na maombi yao.

Kwa upande wa Mufti Dkt. Abubakary Zuberi bin Ally amempokea Makonda na kumfanyia dua maalum,  pia kuahidi kuendeleza ushirikiano huo na kumuombea ili kuhakikisha anafanya kazi zake vyema kwa lengo la kumsaidia Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa manufaa ya Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

About The Author

(Visited 65 times, 1 visits today)

Last modified: December 1, 2023

Close