Visit Sponsor

Written by 2:18 pm KITAIFA Views: 38

KIHENZILE AITEMBELEA TAA, ATOA MAELEKEZO KWA WIZARA YA UCHUKUZI

Naibu Waziri Uchukuzi David Kihenzile ameitaka mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) kupeleka taa za kuongoza ndege katika maeneo ambayo yanatajwa kuwa ni malango makuu ya utalii akiwekea mkazo Arusha na Iringa.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam na menejimenti ya Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) , amesema Tanzania ni yapili kwakuwa na vivutio vyingi vya utalii duniani ambapo asilimia themanini ya watalii hupita kaskani huku Arusha ikitumika kama lango hivyoo taa hizo ni muhimu zikifungwa katika uwanja wa ndege wa Arusha.

Kwa upande mwingine, ameagiza kushughulikiwa kwa malalamiko ya mara kwa mara kuhusu mizigo ya abiria kuchanganywa na mingine kupotea na wakati mwingine kuwasumbua abiria kwenye ufuatiliaji wa mizigo yao na kuutaka uongozi wa mamlaka hiyo kuwabaini wanaosababisha changamoto hiyo na kuwachukulia hatua.

Pamoja na hayo amezitaka taasisi zilizopo chini ya wizara yake kukamilisha miradi kwa wakati pamoja na kuzingatia zaidi mnyororo mzima wa thamani katika miradi hiyo huku wakihakikisha wanalinda maslahi ya watumishi /vibarua wanaofanyakazi katika miradi inayotekelezwa na wizara hiyo.

Vilevile Kihenzile ameielekeza mamlaka hiyo kushughulikiwa malalamiko kuhusu ucheleweshwaji wa abiria katika eneo wanalopita wageni mashuhuri unaosababishwa na utaratibu wa malipo uliowekwa eneo hilo unaosababisha foleni kutokana na mfumo wa makipo unaoelezwa kuwa sio rafiki.

Kwa upande mwingine amezitaka taasisi zilizopo chini ya wizara yake kuweka utaratibu mzuri wa kutekeleza maelekezo ya viongozi wa Serikali kwa kuwa na mfumo wa ufuatiliaji na utekelezaji wa maelekezo hayo.

Kihenzile amesema yapo maagizo mengi hutolewa na viongozi mbalimbali ila utaratibu uliopo hivi sasa hakuna ufuatiliaji makini wa maagizo hayo hivyo ameilekeza Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania kuhakikisha inawasilisha wizarani taarifa kamili ya maelelekezo yote na utekelezaji wake yaliyotolewa na viongozi kwa nyakati tofauti.

Sambamba na hilo Kihenzile amependekeza kwenye kila sekta kiainishwr kitengo ambacho kitasimamia ufuatiliaji wa maagizo na maelekezo ya viongozi yanayotolewa kwa wizara ya Uchukuzi.

Amewataja viongozi hao kuwa ni pamoja na Rais, Makam wa Rais, Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Sekta pamoja na Viongozi wakuu wa Chama cha Mapinduzi.

Aidha, Kihenzile amezitaka taaisi zote chini wa wizara ya uchukuzi kushughulika ipasavyo na kuwa na taarifa za kina kwa maagizo yote ya Bunge, Kamati za Bunge, Repoti ya CAG na Bodi za taasisi.

About The Author

(Visited 38 times, 1 visits today)

Last modified: October 10, 2023

Close